KITAIFA

KIKWETE AWAPONGEZA VIONGOZI WA HALMASHAURI WILAYA YA BAGAMOYO KWA KUSIMAMIA NA KUWAHUDUMIA VIZURI WALENGWA WA TASAF

KIKWETE AWAPONGEZA VIONGOZI WA HALMASHAURI WILAYA YA BAGAMOYO KWA KUSIMAMIA NA KUWAHUDUMIA VIZURI WALENGWA WA TASAF

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama baadhi ya bidhaa za walengwa wa TASAF katika Kata ya Dunda, Kijiji cha Dunda, Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bagamoyo kwa kusimamia na kuwahudumia vizuri walengwa wa
Mradi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaosimamiwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao kwa asilimia kubwa umeinua maisha
ya wananchi wa eneo hilo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Dunda, Kijiji cha Dunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Mhe. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na
walengwa wa TASAF wa Kata ya Dunda, Kijiji cha Dunda katika
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
“Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora niwapongeze ninyi
viongozi wa Halmashauri ya Bagamoyo kwa kujitoa kwenu katika
kuwasimamia na kuwahudumia wananchi wa eneo hili la Bagamoyo,” Mhe.
Kikwete amesema.

Sehemu ya wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Dunda, Kijiji cha Dunda, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akizungumza nao alipokuwa kwenye ziara ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri hiyo.

Mhe. Kikwete amesema kuwa, endapo halmashauri zote nchini Tanzania
zitasimamia na kuratibu mradi wa TASAF kwa usahihi kama ambavyo
halmashauri ya Bagamoyo inafanya, ifikapo mwaka 2026 nchi ya Tanzania
itakuwa imeondokana na tatizo la wananchi kuwa na hali duni za maisha.
Aidha, Mhe. Kikwete amewataka wananchi na walengwa wa halmashauri
ya Wilaya ya Bagamoyo kumuombea Rais Mhe. Dkt. Samia Hassan kwa
kuwa anafanya kazi kubwa ya kuhakikisha kila mwananchi anainuka
kutoka katika hali duni na kuwa na maisha bora.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Shauri Selenda akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza na wanachi na walengwa wa TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Kwa upande wake, mlengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo, Bi. Mwanahawa Sobbo ameishukuru TASAF kwa kumuinua
kimaisha na kumuunganisha na vikundi ambavyo vimemsaidia kupata
mkopo wa Halmashauri ya Wilaya ambao umewawezesha kununua
machine ya boti inayofanya biashara na kuwaingizia kipato kikubwa.

Mlengwa wa TASAF, Bi. Mwanaheri Maulidi akitoa ushuhuda kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete namna TASAF ilivyomsaidia kuinua maisha yake wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.


Naye, Mlengwa mwingine wa TASAF, Bi. Mwanaheri Maulidi ametoa
shukrani kwa Serikali kupitia mradi wa TASAF kwa kuinua maisha yake
kwani ruzuku ambayo alikuwa akiipokea ilimuwezesha kusomesha watoto
wake pamoja na kupata ada yake ya kwenda kujifunza ufundi cherehani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amehitimisha ziara yake ya kikazi katika
Mkoa wa Pwani iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma,
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao pamoja na kukagua
utekelezaji wa Miradi ya TASAF.

About Author

Bongo News

3 Comments

    When we look at how sex dolls affect society, 最 高級 ダッチワイフit’s clear they’re changing how we interact. For some people

    The use of a high-angle shot coupled with extreme soft focus works to create just such a sensation.To see Alex framed with such film techniques gives viewers a felt sense of what dissociation feels like on a phenomenological level.ラブドール 通販

    Gameworld Barbarossa is a treasure hunter’s dream come true. Embark source on an epic quest filled with hidden riches, bonus rounds, and legendary wins inspired by the pirate’s golden age.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *