MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman Kinana, leo Agosti 24, 2023, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa taasisi ya Marekani ya NDI inayojishughulisha na masuala ya demokrasia, Balozi Derek Mitchel, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam. Balozi Mitchel ameipongeza serikali ya CCM kwa hatua nzuri iliyopigwa katika kukuza demokrasia nchini Tanzania. Makamu Mwenyekiti Ndugu Kinana amemhakikishia kiongozi huyo kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania itaendelea kufanya mageuzi yatakayoimarisha demokrasia nchini.

1 Comment
Let’s take a moment to reflect on the past and present of this latest upgradeラブドール オナニー.