Mhandisi Rogatus Hussein Mativila
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewateua wafuatao:-
i) Amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
ii) Amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS). Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi
wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (CASSOA).
Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila
ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.
iii) Amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa
ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge na Uratibu); na
iv) Amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Uteuzi huu umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
2 Comments
ラブドールThank you for making this topic so engaging and easy to grasp.Your article on [specific topic] is incredibly relevant and timely.
エロ ラブドールSaint Paul de Vence,and Grasse,