📌 Dkt. Biteko asema Serikali inatambua jitihada za Asasi za Kiraia kutoa huduma za kisheria kwa Wananchi
📌 Rais Samia apongezwa kwa mageuzi katika huduma za sheria nchini
📌 Wanasheria wakumbushwa kuwa marafiki wa Mungu badala ya Mahakama
📌 Dkt. Biteko ataja mikakati ya Serikali kuhakikisha huduma bora za sheria zinawafikia wananchi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Mawakili wa Serikali kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma na haki ili kusaidia Watanzania sambamba na kuwa washauri wazuri kwa viongozi wao.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 15, 2025 jijini Dodoma wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali.
“Ombi langu kwenu Mawakili wa Serikali fanyeni kazi yenu kwa kuzingatia taaluma yenu ya sheria na haki, ni wajibu wenu kushauri kwa haki na fanyeni kazi bila kuogopa,” amesema Dkt. Biteko

Amesisitiza “Fanyeni kazi ya kutetea Serikali yenu, nendeni mkaishauri Serikali na wakati wote mkatende haki, ifanyeni haki kuwa rafiki yenu na anayetokea mbele yenu aone haki imetendeka hata watakaopotoka wakihukumiwa waone wanastahili hukumu waliyopewa,”
Halikadhalika Dkt. Biteko amewapongeza Mawakili hao wa Serikali pamoja na wadau mbalimbali kwa kuunda na kuendesha Kamati za Ushauri wa Kisheria za Mikoa na Wilaya pamoja na kuendesha Kliniki za Ushauri wa Kisheria bila malipo katika mikoa mitatu ya Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza.
Vilevile, amesema kuwa Serikali inatambua jitihada zinazofanywa na Asasi za Kiraia, na binafsi katika kuwahudumia wananchi kupata huduma za kisheria. Ametaja asasi na vyama hivyo kuwa ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society), Legal and Human Rights Centre (LHRC), Tanzania Legal Aid Providers (TANLAP), Legal Service Facility (LSF), Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) pamoja na Watoa Huduma za Msaada wa kisheria kama UNDP na UN Women.

Ametaja baadhi ya jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya sheria nchini kuwa kuajiri Maafisa Sheria, Mawakili wa Serikali pamoja na Mahakimu na imekuwa ikiwawezesha watoa huduma za kisheria kwa kuanzisha Huduma za Msaada wa Kisheria, uanzishwaji wa Kamati za Ushauri wa Kisheria, Kliniki za Ushauri wa Kisheria pamoja mafunzo kwa wataalamu wa sheria, ujenzi wa maeneo ya kutolea huduma za kisheria kwa lengo la kuhakikisha huduma bora inawafikia wananchi.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amemuelekeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushughulikia changamoto mbalimbali za Chama hicho cha Mawakili wa Serikali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kupata eneo la kujenga Makao Makuu ya Chama na Vivutio vya Mafunzo kwa Mawakili wa Serikali katika mikoa ya Arusha na Dodoma
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni. Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia ameimarisha sekta ya sheria kwa kutekeleza masuala mbalimbali mfano kusaidia uwepo wa haki jinai na Kampeni ya Msaada wa Sheria ya Mama Samia.

Mhe. Kabudi amesema kuwa umuhimu wa mkutano huo wa Mawakili wa Serikali kuwa ni kutoa fursa kwao ya kukutana na kujadiliana masuala ya kitaaluma, maslahi yao pamoja na kufahamiana.
Amewapongeza waasisi wa Chama hicho kwa kujenga taswira nzuri huku akiwaasa viongozi wengine watakao fuata kuendeleza taswira hiyo na amewataka mawakili hao kuwa marafiki wa Mungu badala ya Mahakama kwa kutenda haki na kusema kweli wakati wa kutimiza majukumu yao.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamza Johari amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kukilea chama hicho kwa miaka mitatu na kusema kuwa ni wajibu wao sasa kukilinda na kuhakikisha kinafikia malengo yake.

Pia, amebainisha kuwa kupitia mkutano huo wameidhinisha Mpango Mkakati wa Chama hicho kitakachoufuata na kutekeleza katika kipindi cha miaka mitano.
“Tumetengeneza Mpango Mkakati tunaokwenda kuutekeleza kwa shauku kubwa pamoja na viongozi wapya watakao chaguliwa katika Uchaguzi unaofanyika leo,” amesema Mhe. Johari.
Amesema hadi kufikia Aprili 9, 2025 idadi ya Mawakili wa Serikali waliojisajiliwa katika Daftari la Mawakili wa Serikali imefikia 3,760 kutoka 2,652 waliosajiliwa wakati wa kuanzishwa kwa Chama hicho.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar, Mhe. Dkt. Mwinyi Talib Haji amewaomba Mawakili na Maafisa Sheria wa Serikali kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria ili kujenga jamii imara na kupunguza mizozo katika jamii.

Aidha, amesema taasisi za sheria ziendelee kushirikiana ili kusaidia wananchi na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi za kuhudumia jamii na kuleta ustawi kwa mustakabali kwa maendeleo ya nchi.
Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali, Amedeus Shayo amesema kuwa Chama chao kimefanikiwa kujenga mfumo wa kielektoniki wa kukusanya ada kwa wanachama pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi zinazoshughilika na masuala ya sheria za ndani na nje ya nchi.
“ Rais Samia ameendelea kuwa kielelezo kizuri cha haki kupitia Kampeni yake ya Msaada wa Kisheria na Mawakili wanashiriki kutoa huduma za sheria kwa wananchi. Pia, agizo la Rais Samia la Mawakili kuwa walinzi wa uchumi wa nchi kwa kutumia kalamu limeweka msingi wa Chama hiki na umesaidia kuboresha sheria kadhaa mfano Sheria ya Uwekezaji,” amesema Shayo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu na Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia kwa kuzindua Chama hicho mwaka 2022 na kusema “ Chama hiki kama kilivyoanzishwa na malengo yake kitabaki kuwa Chama bora cha kitaaluma kwa sababu Serikali na mawakili walijipanga kuwa nacho na hili ni jeshi la kulinda uchumi wa nchi kwa sheria na kalamu,”
Mkutano huo uliohudhuriwa na Mawakili wa Serikali kutoka katika Wizara, Wakala na Taasisi za Serikali, Mashirika ya umma umeongozwa na Kauli mbiu “ Utawala wa Sheria katika Utekelezaji wa Majukumu ya Serikaki ni Nguzo Muhimu katika Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”
36 Comments
Interesting read! Do you have any tips for beginners on this?
аристон хотпоинт ремонт сервисный центр ariston
kamagra en ligne: Acheter Kamagra site fiable – achat kamagra
vente de mГ©dicament en ligne: Livraison rapide – pharmacie en ligne sans ordonnance pharmafst.com
cialis sans ordonnance: Acheter Cialis 20 mg pas cher – Acheter Cialis tadalmed.shop
Achat mГ©dicament en ligne fiable: pharmacie en ligne sans ordonnance – pharmacie en ligne fiable pharmafst.com
pharmacies en ligne certifiГ©es pharmacie en ligne pharmacie en ligne fiable pharmafst.shop
Acheter Kamagra site fiable: kamagra gel – achat kamagra
https://kamagraprix.com/# kamagra pas cher
pharmacie en ligne france livraison internationale: Livraison rapide – pharmacies en ligne certifiГ©es pharmafst.com
pharmacie en ligne pas cher Pharmacies en ligne certifiees Pharmacie en ligne livraison Europe pharmafst.shop
Cialis en ligne: cialis prix – Cialis en ligne tadalmed.shop
Acheter Kamagra site fiable: kamagra pas cher – kamagra pas cher
https://kamagraprix.com/# kamagra oral jelly
Achetez vos kamagra medicaments: kamagra pas cher – kamagra livraison 24h
Kamagra Oral Jelly pas cher: Acheter Kamagra site fiable – kamagra oral jelly
Achat Cialis en ligne fiable Pharmacie en ligne Cialis sans ordonnance Tadalafil achat en ligne tadalmed.com
http://pharmafst.com/# Achat mГ©dicament en ligne fiable
Pharmacie Internationale en ligne: Meilleure pharmacie en ligne – pharmacie en ligne sans ordonnance pharmafst.com
Tadalafil sans ordonnance en ligne: Achat Cialis en ligne fiable – Achat Cialis en ligne fiable tadalmed.shop
Cialis generique prix Achat Cialis en ligne fiable cialis generique tadalmed.com
http://kamagraprix.com/# Kamagra Commander maintenant
pharmacie en ligne france pas cher: Pharmacie en ligne France – pharmacies en ligne certifiГ©es pharmafst.com
pharmacie en ligne livraison europe: Medicaments en ligne livres en 24h – Pharmacie Internationale en ligne pharmafst.com
Acheter Viagra Cialis sans ordonnance: Achat Cialis en ligne fiable – Acheter Cialis tadalmed.shop
kamagra gel kamagra oral jelly Achetez vos kamagra medicaments
https://tadalmed.shop/# Tadalafil 20 mg prix en pharmacie
Tadalafil achat en ligne: Cialis en ligne – Cialis sans ordonnance 24h tadalmed.shop
п»їpharmacie en ligne france: Pharmacies en ligne certifiees – vente de mГ©dicament en ligne pharmafst.com
https://tadalmed.shop/# Cialis generique prix
Pharmacie sans ordonnance Meilleure pharmacie en ligne pharmacie en ligne avec ordonnance pharmafst.shop
Cialis sans ordonnance pas cher: Acheter Cialis – cialis sans ordonnance tadalmed.shop
https://pharmafst.com/# pharmacie en ligne avec ordonnance
Pharmacie Internationale en ligne Pharmacie sans ordonnance pharmacie en ligne sans ordonnance pharmafst.shop
achat kamagra: kamagra livraison 24h – Kamagra pharmacie en ligne
Cialis en ligne: Cialis sans ordonnance pas cher – Cialis sans ordonnance 24h tadalmed.shop