KITAIFA

NDEJEMBI ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI WA SHULE ZINAZOJENGWA KATA YA MANCHALI CHAMWINO

NDEJEMBI ASHIRIKIANA NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI WA SHULE ZINAZOJENGWA KATA YA MANCHALI CHAMWINO

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Deogratius Ndejembi ameshirikiana na wananchi wa kata ya Manchali
kuchimba msingi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Manchali itakayoitwa
Ndejembi pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa
Dodoma inayojengwa katika kata hiyo kupitia mradi wa SEQUIP.
Mhe. Ndejembi amesema, wananchi wa Kata ya Manchali wanashiriki
kikamilifu katika ujenzi wa shule hizo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono
jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan za kuboresha elimu nchini.


Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, ushiriki wa wananchi unapunguza
gharama za ujenzi na kuongeza kuwa lengo lake ni kuhakikisha shule ya
Sekondari ya Ndejembi inakamilika na fedha inabaki, ikizingatiwa kuwa
wananchi wamempa heshima kwa kuipa shule hiyo jina lake kwa kuthamini
mchango wake.
Akizungumzia jitihada za kupunguza gharama ya ujenzi katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana inayojengwa, Mhe. Ndejembi amesema uongozi
wa halmashauri umemtafuta mzabuni wa kufyatua tofali ambaye
amefungua kiwanda cha kufyatua tofali kwa gharama nafuu ya shilingi
1400 kwa tofali kwenye eneo ambalo shule hiyo inajengwa.
Aidha, Mhe. Ndejembi amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kutoa fedha za kujenga wa shule hizo katika kata ya Manchali,
shule ambazo zitatatua changamoto ya wanafunzi wa eneo hilo na maeneo
jirani kutembea umbali mrefu ili kupata elimu.


“Rais Samia tangia aingie madarakani amefanya mambo makubwa kwa
wananchi wa jimbo la chamwino kwani kila eneo ametoa fedha za ujenzi
wa miundombinu ya elimu kwa ajili ya kutatua changamoto ya wanafunzi
kutembea umbali mrefu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Dkt. Charles Msonde amewapongeza wananchi wa Manchali kwa kushiriki
kuchimba msingi wa shule za sekondari zinazojengwa na kuongeza kuwa,

ushiriki wao ni ishara ya kuunga mkono kwa vitendo jitihada za
Mheshimiwa Rais kuboresha elimu nchini.

About Author

Bongo News

2253 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *