Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa Amiry Mkufya maarufu Amesco amepita katika vijiwe vya bodaboda na kwenye mikusanyiko ya watu kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kabla ya zoezi kufungwa february 19 ndani ya mkoa wa Tanga.

Mkufya amepita katika vijiwe hivyo vya bodaboda leo katika Halmashauri ya Lushoto Jimbo la Mlalo Mkoani Tanga.
Amesema kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu ni muhimu sababu inamuwezesha mwananchi kupata haki ya kumchagua kiongozi anayemtaka wakati wa uchaguzi.

” Tukiboresha taarifa zetu katika daftari la mpiga kura zitatusaidia kuwezesha kumchagua Rais Samia, Madiwani na Wabunge tunaowataka” Amesema Mkufya Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa kupitia wilaya ya Lushoto.
1 Comment
Your blog consistently engages my attention from beginning to end. I cannot stop reading without devouring every word you write.