Awapa darasa wanaodai sababu ya CCM kupitisha wagombea Urais

  • Asema yupo tayari kuwapa somo waifahamu vyema katiba ya Chama  

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mainduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, uliomchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kugombea kiti cha Urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umezingatia takwa la kikatiba na mamlaka ya Mkutano Mkuu.

Amesema baadhi ya watu wanaojiita wanaCCM wanaodai kwamba bado hawajaelewa sababu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kupitisha uamuzi huo, atawasaidia kuelewesha kwani uwezo wa binadamu kufahamu jambo hauwezi kulingana.

Wasira aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati viongozi, wanachama,  wapenzi wa CCM na wananchi kutoka maeneo mbalimbali walipojitokeza kumpokea.

“Baada ya Mkutano Mkuu kutambua kazi kubwa zilizofanywa na serikali zote mbili, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar, Mkutano Mkuu wa CCM ukasema kama hali ni hii kuna sababu gani kuchelewesha kutangaza mgombea?.

“Sasa wapo watu wanaosema wao ni wanachama wa CCM, hawakuelewa. Hilo nalo siyo jambo la ajabu. Tutawasaidia kuelewa maana siyo watu wote wanaweza kuelewa sawa. lakini tunawaambia Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo kikao kikuu cha mwisho,” amesema.

Wasira ameeleza kuwa Mkutano Mkuu wa Chama una mamlaka ya kubadili, kufuta na kurekebisha uamuzi wowote uliofanywa na kikao cha chini yake, kufuta maamuzi yaliyofanywa na kiongozi yeyote wa CCM.

Amesisitiza: “Sasa aliye na mashaka katika jambo hilo kama wote hawawezi aje kwangu nitamsadia maana katiba ipo kichwani. Uamuzi tulioufanya umezingatia Katiba ya CCM ibara ya 101 inayotutaka tuchague jina moja la kuwa mgombea wa kiti cha Urais, tulitumia ibara hiyo na kwa mamlaka ya Mkutano Mkuu ameteuliwa Dk. Samia.”

About Author

Bongo News

3 Comments

    c49zzh

    buy now pay later in nigeria
    Get a quick loan in Nigeria in 2 Minutes. Migo helps small businesses extend low-interest, no collateral micro loans, banking services and credit purchase to their customers. With Migo’s microlending APIs, SMEs, FinTechs, Banks, Telcos and Retailers in Nigeria can support their customers with:

    1. Access to required loan amounts at the point of need

    2. Low interest rates on quick loans and credit products

    3. Flexible and easy repayment options

    4. Personalized financial services and products across website, mobile app, USSD, SMS, ATM, POS, Whatsapp, Facebook, Twitter and Instagram

    ¡Comercializamos sistemas de balanceo!
    Somos creadores directos, elaborando en tres países a la vez: España, Argentina y Portugal.

    Nuestros productos son de altísima calidad, y como no actuamos como intermediarios, sino productores directos, nuestro coste es más competitivo que el de nuestros competidores.

    Realizamos envĂ­os a todo el mundo, lea la descripciĂłn de nuestros sistemas de balanceo en nuestra web.

    El dispositivo de balanceo es portátil, ligero, lo que permite balancear todo tipo de rotores en distintos ambiente.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *