Raisa Said, Tanga

Zaidi ya wakazi million 1.4 wa Mkoa wa Tanga wanatarajiwa kujiandikisha katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura linaloanza rasmi oktoba 11 hadi oktoba 20 nchini kote

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akizindua zoezi hilo la uandikishaji linaloanza rasmi kesho oktoba 11.

Balozi Burian alisema zoezi hilo litaanza rasmi oktoba 11 katika vituo 5199 vilivyopo katika mkoa mzima wa Tanga.

” Mkoa wa Tanga una Mamlaka za miji midogo mitatu , Kata 245, Mitaa 270, Vitongo 4528 na vijiji 763″ Alisema Mkuu wa Mkoa huyo . Alisema mkoa una vituo vya ziada 500 katika idadi ya jumla ya vituo vyote vya mkoa.

Mkuu wa Mkoa huyo pia alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi na wakazi wote wa mkoa wa Tanga wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftari la mpiga kula litakaloandikishwa kwa siku 10 ndani ya vituo vyote vilivyotengwa ndani ya mkoa huu.

Alipongeza vyombo vya habari kwa kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya zoezi hilo na kuvitaka viendelee kufanya hivyo.

Hata hivyo Mkuu wa mkoa huyo alisisitiza kuwa baada ya kujiandikisha wananchi watapata fursa ya kukagua orodha ya wapiga kura kwa siku saba tangu tarehe y kubandikwa kwenye eneo alilojiandikishia.

Uchaguzi wa Serikali za Miitaa unatarajiwa kufanyika nchini kote November 27 mwaka huu.

Mwisho

About Author

Bongo News

33 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *