Mjadala wa Bunge la Ulaya (EU) kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu umefanyika jana na kutoa maazimio sita kwa Tanzania kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025.

Pamoja na mambo mengine, azimio hilo limetaka Kesi ya Lissu kuendeshwa kwa uwazi, na Mamlaka za Tanzania kulinda uhuru wa kisiasa, usalama wa waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, na wanaharakati wanaotetea ushoga.

Aidha Bunge hilo limetaka, CHADEMA iruhusiwe kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu licha ya kwamba chama hicho hakisaini kanuni za Tume ya uchaguzi.

Bunge hilo limeagiza EU na nchi zake kufuatilia kwa karibu kesi hiyo ya Lissu na jinsi Tanzania inavyolinda haki za binadamu, waandishi na wapenzi wa jinsia moja.

Taarifa ya kikao hicho cha Bunge la Ulaya na maazimio yake imesambazwa jana Mei 7, saa chache baada ya kumalizika kwa kikao hicho.

About Author

Bongo News

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *