KITAIFA

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI MHA. GODFREY KASEKENYA WAKATI WA UTIAJI SAINI MIKATABA MINNE YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MABASI YA HARAKA (BRT) DAR ES SALAAM

HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI MHA. GODFREY  KASEKENYA WAKATI WA UTIAJI SAINI MIKATABA MINNE YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA  MABASI YA HARAKA (BRT) DAR ES SALAAM

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

  1. Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, kwa kutujalia afya njema na kukutana hapa leo. Naomba niwashukuru sana kwa kuwa pamoja nasi katika Hafla ya Utiaji Saini Mikataba inayohusu Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Usafiri Haraka wa Mabasi (BRT Phase 4), Jijini Dar es Salaam na ujenzi wa barabara ya TAMCO – Vikawe hadi Mapinga kwa kiwango cha lami; sehemu ya Pangani hadi Mapinga (Km 13.59).

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

  • Kati ya mikataba ya BRT inayosainiwa leo, mikataba mitatu inahusu Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu Awamu ya Nne (BRT Phase 4) kutoka Maktaba mpaka Tegeta DAWASA. Vilevile, mkataba mmoja unahusu Uboreshaji wa Miundombinu ya BRT iliyojengwa Awamu ya Kwanza katika Barabara ya Morogoro ambapo upanuzi utafanyika wa sehemu ya barabara kutoka Ubungo mpaka Kimara yenye urefu wa Km 5 kutoka njia Sita (6) za sasa kwenda Njia Nane (8), kujenga njia za watembea kwa miguu na barabara za pembeni (service roads) na kuboresha makutano ya barabara kwa kuimarisha barabara za kuwezesha wanaopinda kulia na wanaozunguka kurudi walikotoka (loop roads). Pia, inahusisha kuweka ngazi kwenye madaraja ya wapita kwa miguu eneo la Kimara na Morocco ili kuweka njia mbadala na kuvutia watumiaji wengi zaidi.

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

  • Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu Awamu ya Nne, (BRT Phase 4) ni sehemu ya Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi (BRT) uliobuniwa na Serikali mwaka 2004 chini ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari na kuongeza tija katika shughuli za kiuchumi kwa kupunguza muda na gharama za kusafiri. Mpango mkakati wa mradi huu umeendelea kuboreshwa na umeainisha barabara ambazo zitajengwa kwa awamu sita (6) kama ifuatavyo:
  • Awamu ya kwanza imekamilika na ilihusu ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa km 21.4 kutoka katikati ya Jiji hadi Kimara ikiwa na matawi mawili ya barabara za Magomeni hadi Morocco na Fire hadi Kariakoo. Mradi huu ulikamilika mwaka 2016 na unafanyakazi vizuri.
  1. Awamu ya Pili ni ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa km 20.3 kutoka katikati ya jiji hadi Mbagala ambayo ujenzi wake unaendelea na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
  1. Awamu ya Tatu ni ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa km 23.33 kutoka katikati ya jiji, hadi Gongolamboto. Ujenzi umeanza Agosti, 2022 na unategemewa kukamilika ndani ya miezi 24. Mradi huu unagharimiwa kupitia program ya Dar es salaam Urban Transport Project (DUTP).
  1. Awamu ya Nne ni ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa km 29.13 ambayo tunashudia utiaji saini leo na inahusisha barabara kutoka katikati ya jiji hadi Tegeta DAWASA; pamoja na kipande cha kutoka Mwenge hadi Ubungo. Mradi huu unagharimiwa kupitia program ya Dar es salaam Urban Transport Project (DUTP).
  • Awamu ya Tano ni ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa km 27.6 kutoka Ubungo hadi Bandari; pamoja na kipande cha barabara ya Tabata kutoka Segerea hadi Kigogo na sehemu ya Barabara ya Mbagala. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la maendeleo la Ufaransa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
  • Awamu ya Sita ni ujenzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa km 26.5 ambayo itahusisha barabara ya Mwai Kibaki kutoka Morocco hadi Kawe (Km. 7), barabara ya Kimara hadi Kibamba (Km 14) na Mbagala hadi Vikindu (Km. 5.5).

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

  • Miradi mingine ambayo imetekelezwa kwa kugharamiwa na Serikali ikishirikiana na Benki ya Dunia kupitia program ya Dar es salaam Urban Transport Project (DUTP) ni kama ifuatavyo:
  • Ujenzi wa Daraja la Juu la John Kijazi na ujenzi wa Karakana ya Mabasi ya BRT eneo la Ubungo palipokuwa na Kituo cha Mabasi ya Mikoani; na
  • Usanifu wa Daraja la Jangwani kutoka eneo la “Fire” kwenda Magomeni Mapipa.

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

  • Napenda kuwashukuru washirika wa Maendeleo, hususani Benki ya Dunia ambayo inagharimia miradi inayosainiwa leo kupitia program ya Dar es salaam Urban Transport Project (DUTP) kwa kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata Minudombinu bora ya usafiri.
  • miundombinu hii ya BRT ni kuwaondolea wananchi kero ya usafiri wa barabarani, kupata usafiri wa haraka na kupunguza gharama za safari ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji, hivyo kukuza uchumi wa wananchi pamoja na nchi yetu.
  • . Vilevile itasaidia katika kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii na kukuza utalii katika Jiji letu la Dar es Salaam kwa ujumla.

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

  1. na mkataba mmoja wa ujenzi wa barabara ya TAMCO – Vikawe hadi Mapinga kwa kiwango cha lami; sehemu ya Pangani hadi Mapinga (Km 13.59) ambao utajengwa kwa gharama ya Shilingi TZS 17,859,098,225.00, bila kujumuisha kodi ya ongezeko la thamani (18% VAT) ya Shilingi TZS 3,050,837,680.50.
  1. Gharama ya Ujenzi wa miradi hii ni kubwa hivyo naomba tuzingatie thamani ya fedha ya mradi (Value for Money) wakati wa ujenzi. Naiagiza TANROADS kusimamia miradi hii kwa udhibiti mkubwa ili barabara pamoja na daraja la Mwiti viweze kutumika kwa muda uliopangwa (Design Life).

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

  1. Vilevile, Ninaomba tuwape ushirikiano Makandarasi walioko kwenye miradi mbalimbali, hususan Makandarasi watakaofanya kazi ya ujenzi wa miradi hii. Aidha, napenda kutoa shukrani za dhati kwa viongozi na wananchi walioko kwenye maeneo ya miradi mingine kwa ushirikiano wanaowapa Makandarasi. Hata hivyo, napenda nitoe rai juu ya ulinzi wa mali za miradi na vifaa vitakavyo tumika katika ujenzi. Tuwasisitize wananchi wetu wanao zunguka maeneo ya miradi kuepukana na uhalifu wa namna yoyote kwa vifaa vya Ujenzi katika miradi, badala yake wavilinde. Hii itasaidia kulinda thamani halisi ya miradi lakini pia kukamilika kwa wakati na ubora unaokubalika.
  2. Mwisho napenda kuwashukuru Viongozi wote wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa mapokezi mazuri mlionipa mimi na wenzangu, nasema asanteni sana.
  1. Baada ya kusema haya machache naomba niwakushukuru sana kwa kuwa pamoja nasi katika hafla hii fupi nasema asanteni sana.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *