KIMATAIFA KITAIFA

SPIKA DK TULIA AZIDI KUIPAISHA TANZANIA, SASA AIPELEKA MOROCCO

SPIKA DK TULIA AZIDI KUIPAISHA TANZANIA, SASA AIPELEKA MOROCCO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Spika wa Bunge la Morocco, Rachid Talbi El Alami katika ofisi za Bunge hilo zilizopo Jijini Rabat nchini Morocco leo Septemba 18, 2023.

Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mabunge ya nchi hizo mbili hususani katika sekta ya kilimo, viwanda na biashara.

Aidha, Dkt. Tulia ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Serikali ya Morocco kwa vifo vya watu zaidi ya 3000 na madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mapema mwezi huu.

Pia amepongeza juhudi zilinazofanywa na Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco katika kukabiliana na maafa pamoja na changamoto zilizotokana na tetemeko hilo.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *