Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua Tuzo ya Ubunifu ambayo itahusisha mawazo ya Ubunifu kutoka kwa Watanzania kuhusu namna bora ya kuongeza wigo wa Kodi kwa kuainisha vyanzo vipya vya Kodi.

Uzinduzi huo umefanywa tarehe 08.05.2025 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanislaus Nyongo wakati wa Kongamano la kwanza la Kodi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Naibu Waziri Nyongo amesema kupitia Tuzo hiyo TRA itapata mawazo mapya kutoka kwa Watanzania ambayo yatasaidia kuongeza wigo wa Kodi kwa kuainisha namna bora ya kukusanya Kodi sambamba na vyanzo vipya vya Kodi.

“Tunao Vijana wengi wabunifu waliomaliza vyuo vikuu, hii ni fursa kwenu ichangamkieni mpate hizo tuzo lakini pia msaidie nchi yenu katika masuala ya kukusanya Kodi kwa maendeleo ya kila mmoja wetu na vizazi vijavyo” amesema Nyongo.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo imetenga kiasi cha Shilingi milioni 200 kwaajili ya kazi hiyo ambapo watakaotoa mawazo Bora zaidi yatakayokuwa na Tija, watapatiwa kuanzia Sh. Milioni 20.

Amesema zoezi hilo la kupokea mawazo kwaajili ya kuongeza wigo wa Kodi litaaanza rasmi tarehe 09.05.2025 na kuhitimishwa tarehe 15.06.2025 ambapo wale watakaokuwa wametoa mawazo bora zaidi watatangazwa.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kuchangamkia fursa hiyo ya kuisaidia nchi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *