Maoni ya Patrick Mutabazi Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa nchi Tanzania.

Kuna Matukio yakitokea katika nchi, namna yanavyotokea, yanavyosambaa haraka na habari zake zinavyoandikwa na mijadala yake unagundua kabisa ni Mkakati.

Padre Kitima amekuwa Katibu Mkuu wa TEC kwa muda mrefu, amekuwa kiongozi wa kiroho wa Kanisa ambaye ameshiriki kwenye mambo mengi na tofauti na hajawahi kudhuliwa, kutishwa wala kupata tishio la kushambuliwa na kutishiwa maisha yake binafsi. Kwa nini Leo? Kwa nini Kipindi hiki?.

Tukio limetokea Sehemu ambayo ina ulinzi, ina camera za ulinzi na ni sehemu ya Viongozi kiroho na inamilikiwa na Kanisa, anashambuliwaje kiongozi wa Baraza eneo la Kanisa?

Kwa nini Lawama zitupwe upande mmoja wa Serikali wakati kiongozi ameshambuliwa ndani ya Eneo la Kanisa na lenye ulinzi wa Kanisa?

Hatuwezi kufika hitimisho kwamba ni Serikali umehusika kabla ya kujadili maisha ya Padre Kitima, je hana maadui binafsi? Ana Migogoro Binafsi na wenzake ndani ya Kanisa au kwenye maisha ya kawaida ambao wanaweza kutumia nafasi hii tena kipindi hiki kumshambulia na kupoteza Focus kwa kuituhumu Serikali?

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imetoa taarifa ya kushikiliwa mtuhumiwa mmoja kwa tukio hili Baya sana dhidi ya Padre Kitima kwa nini tusisubiri uchunguzi na Upelelezi kukamilika wa tukio hili na watuhumiwa kutajwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Dola kuliko kuanza kurusha lawama na Tuhuma upande mmoja? Je wanaotupa lawama kwa Serikali wana ushahidi Gani Serikali imehusika?

Kipindi ambacho Nchi inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu na kundi kubwa la Wapiga kura ni Wakristo tena Wakatoliki hakuna kiongozi anaweza kuruhusu kushambuliwa kwa Kiongozi wa Kanisa ambalo anategemea waumini wake kumpigia kura.

Rais wetu ni Rais Mwenye Upendo, Unyenyekevu mkubwa, Mwenye hofu ya Mungu na mara zote amekuwa akimtanguliza Mungu kwenye majukumu yake hawezi na hajawahi kuruhusu, kupenda au kutaka kushuhudia Viongozi wa Dini wakijeruhiwa na kushambuliwa.

Rais Samia Suluhu Hassan ndo kiongozi pekee ameweka Rekodi ya Kipekee ya Kutembelea Makao Makuu ya Kanisa Katoliki (TEC) na kuzungumza na Viongozi wa Kanisa hilo kwa kikao cha Siri. Amekuwa akilithamini Kanisa, Akishiriki Matukio mbalimbali ya Kanisa Katoliki moja kwa moja na kutuma wasaidizi wake kwenye matukio yake. Ameshiriki ujenzi wa Kanisa maeneo mbalimbali, amemtembelea Hayati Baba Mtakatifu Francisko Nchini Vatican, ameshiriki Mazishi yake kwa kutuma Makamu wake wa Rais, na mara zote amekuwa Mnyenyekevu mbele ya Kanisa.

Tusimruhusu Rais Samia kuchafuliwa, kugombanishwa na Kanisa na waamini wake na Kikundi kidogo cha watu wenye nia ovu.

About Author

Bongo News

3 Comments

    I’ve been looking for info like this—glad I found your blog.

    kuşadası escort ilan Elit ve bakımlı olan seksi Kuşadası escort bayanları size en özel olacak imkanları da aktarmasını bilir. Bu sebepten dolayı da kendinizi fazlasıyla özel … https://suvanami.com/

    маркетплейс аккаунтов соцсетей https://birzha-akkauntov-online.ru/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *