KITAIFA

BASHUNGWA AUNGANA NA WANAKAGERA KUMKARIBISHA NYUMBANI KARDINALI RUGAMBWA.

BASHUNGWA AUNGANA NA WANAKAGERA KUMKARIBISHA NYUMBANI KARDINALI RUGAMBWA.

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ameungana na wananchi wa wilaya ya Karagwe na Mkoa Kagera katika hafla ya kumpongeza na kumkaribisha nyumbani Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, baada ya kuteuliwa na kusimikwa rasmi na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Kardinali.

Hafla hiyo ilifanyika Disemba 28, 2023 nyumba alipozaliwa katika kijiji cha Kasheshe, Nyaishozi wilayani Karagwe mkoani Kagera na kuhudhuria na viongozi mbalimbali wa wa Dini na Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa, ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Bashungwa alitoa salamu za pongezi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kardinali Rugambwa.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaungana na Watanzania kuendelea kumpongeza Kardinali kwa heshima hii ambayo nchi yetu tumeipata, amenipa dhamana ya Wizara ya Ujenzi na baada ya kuona mawasiliano barabara ya kuja hapa Kasheshe yalivyokuwa, sisi tulijiongeza ili tusimuangushe Rais tukatengeneza barabara ili wageni watakaotoka sehemu  mbalimbali wafike hapa  kwa urahisi kwa kumpongeza Kadinali”- alisema Bashungwa.

Bashungwa alitoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kumuombea Kardinali Rugambwa kheri, afya njema, na mafanikio katika utumishi wake.

Kwa Upande wake,  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa alisema Mkoa wa Kagera una bahati sana kwani umeweza kumtoa Kardinali na hiyo ni heshima ya kipekee ambayo itasaidia mkoa wa Kagera kuwa na wacha Mungu na kuepuka yote yaliyokatazwa kwenye maandiko matakatifu.

“Tuepuke yote yaliyokatazwa ikiwemo uzinzi, kula rushwa, wizi, roho mbaya na uuaji. Tuishi kwa upendo na kutenda yale yanayompendeza Mungu na tukitenda hivyo tutakuwa tumemfurahisha Mungu na tutakuwa tumemfuharisha Kadinali wetu Rugambwa” – alisema RC Mwassa.

Naye,  Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa aliwashukuru wananchi wa Kagera kwa kumpokea na kuwasihi Watanzania kuendelea kumtegemea Mungu kwa kila jambo ili waweze kuvuna mema.

“Tubaki tumejiaminisha kwa Mwenyezi Mungu na akiwa pamoja nasi tunaamini kabisa tunaweza kuyafanya mengi sana katika maisha yetu. Niwasihi tuzidi kumtegemea Mungu ndiye anayetufanya tuendelee kuwepo na ndiye anayefanya tuyapate mengi kupitia kwa wengine ambao ni yeye mwenyewe kawaweka” – alisema Kardinali Rugambwa.

About Author

Bongo News

5 Comments

    Link exchange is nothing else however it is just placing the other person’s
    weblog link on your page at proper place and other person will also
    do same in support of you.

    my web page :: nordvpn coupons inspiresensation

    Hello there, just became aware of your blog through Google, and found that it is truly informative.
    I am going to watch out for brussels. I’ll be
    grateful if you continue this in future. Lots of people will be benefited
    from your writing. Cheers!

    My page :: Nordvpn Coupons Inspiresensation

    It’s an remarkable paragraph for all the internet visitors; they will get advantage from it I am sure.

    Take a look at my blog post nordvpn coupons inspiresensation; t.co,

    Everything is very open with a very clear explanation of the issues.
    It was definitely informative. Your site is useful. Thank you for sharing!

    My web site nordvpn coupons inspiresensation (in.mt)

    350fairfax nordvpn coupon
    Thank you for the good writeup. It in truth used to be a amusement
    account it. Look complicated to more delivered agreeable
    from you! By the way, how could we be in contact?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *