KIMATAIFA KITAIFA

HATI 14 ZA MAKUBALIANO BAINA YA TANZANIA NA INDIA ZASAINIWA

HATI 14 ZA MAKUBALIANO BAINA YA TANZANIA NA INDIA ZASAINIWA

Tanzania na India zimetia saini hati za makubaliano 14 na mkataba mmoja, ambapo hati 10 zimehusisha taasisi za serikali na tano za sekta binafsi.

Katika mkutano wa pamoja na waadhishi wa habari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wameshuhudia makabidhiano ya hati 6 kati ya zile zilizosainiwa ambazo zinajumuisha:

1. Hati ya makubaliano kati ya Wizara ya Elektroniki na Teknolojia ya Habari ya India na Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu ushirikiano katika nyanja ya kupeana suluhu zenye mafanikio za kidijitali zinazotekelezwa kwa ujuzi wa idadi ya watu kwa ajili ya mabadiliko ya kidijitali.

2. Mabadilishano ya Hati ya makubaliano ya kiufundi kati ya Jeshi la Wanamaji la India na Shirika la Wakala wa Meli wa Tanzania kuhusu kupeana taarifa za meli za kibiashara.

3. Hati ya makubaliano ya mpango wa kubadilishana utamaduni kati ya India na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka ya 2023 – 2026.

4. Hati ya makubaliano kati ya Baraza la Michezo la Taifa la Tanzania na Mamlaka ya Michezo ya India kuhusu Ushirikiano katika Sekta ya Michezo.

5. Hati ya makubaliano kati ya Mamlaka ya Bandari ya Jawaharlal Nehru chini ya Wizara ya Usafirishaji wa Bandari na Njia za Majini ya India na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa ajili ya kuanzisha Kongani ya Biashara nchini Tanzania.

6. Hati ya makubaliano kati ya Coaching Shipyard Limited na Marine Services Cooperation Limited kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Usafiri wa Majini

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *