KIMATAIFA KITAIFA

IGP WAMBURA – MAOFISA NA ASKARI KUPATIWA MAFUNZO MAALUM

IGP WAMBURA – MAOFISA NA ASKARI KUPATIWA MAFUNZO MAALUM

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Camillus M.Wambura IGP akiwa na ujumbe wa Maofisa watano kutoka Jeshi la Polisi Tanzania leo Mei 15,2023 wameanza rasmi ziara ya kikazi Nchini Ireland ambapo ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Ireland “An Garda Síochána” na kukutana na Deputy  Commissioner Anne Marie McMahon.Wameweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kubaini,kuzuia na kutanzua  makosa ya jinai hususani Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji dhidi ya watoto.

Pia walipata fursa ya kujadili namna ya kushirikiana kwenye eneo la mafunzo kwa maafisa na askari kati ya Jeshi la Polisi Ireland na Jeshi la Polisi Tanzania. Picha na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi Tanzania.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *