KITAIFA

MWENEZI MAKONDA ATUA IVUMWE SEKONDARI MBEYA, AWEKA JIWE LA MSINGI

MWENEZI MAKONDA ATUA IVUMWE SEKONDARI MBEYA, AWEKA JIWE LA MSINGI

Katibu wa NEC itikadi,uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM) Paul Makonda ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Ivumwe jijini Mbeya.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo Mwenezi Makonda amesisitiza kuhusu kuwalea watoto katika misingi ya maadili mema.

Aidha amezitaka,zaidi shule zinazomilikuwa na jumuiya ya wazazi wa CCM kuwa za mfano kwenye malezi ya watoto kimaadili.

Jumuiya ya wazazi nchini imetangaza kuzifanyia mapitio shule zote za jumuiya hiyo ili kuendana na mazingira ya sasa na kukudhi mahitaji ya kijamii na mahitaji ya soko la ajira duniani.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *