BIASHARA

PANGANI KUFUNGUKA KIUTALII, DKT BITEKO AZINDUA MPANGO WA KUTANGAZA VIVUTIO

PANGANI KUFUNGUKA KIUTALII, DKT BITEKO AZINDUA MPANGO WA KUTANGAZA VIVUTIO

Asisitiza Wakuu wa mikoa, Wilaya kuwa wabunifu kutangaza fursa za utaliii

Awahimiza Watendaji kutimiza wajibu wao kuwahudumia Watanzania

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amezindua mpango mkakati wa kutangaza fursa zilizopo Sekta ya Utalii katika wilaya ya Pangani, mkoani Tanga ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuikuza sekta hiyo nchini.

Dkt. Biteko amefanya uzinduzi huo Oktoba 7, 2023 jijini Dar es salaam katika Kongamano la Uwekezaji la Swahili International Tourism Expo lenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko katika wilaya hiyo ikiwemo utalii katika mbuga ya Saadani, fukwe, kilimo biashara pamoja na uchumi wa Buluu katika wilaya hiyo.

Amesisitiza kuwa, Kongamano hilo litumike kuitangaza wilaya ya Pangani na kubadilishana mawasiliano ili fursa zilizoko Pangani ambazo hazipatikani kwengine zishawishi watu wengine kuzifuata.

“Niwapongeze sana watu wa Pangani kupitia Mkuu wa wilaya kwa ubunifu huu wa hali ya juu na nitoe wito kwa wilaya zingine kuiga Pangani na kufungua fursa za utalii na uwekezaji kwenye wilaya zao” Amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesema kuwa, sekta ya utalii kwa sasa mchango wake katika Pato la Taifa ni asilimia 17. Amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira rafiki katika sekta hiyo ili kuendelea kuvutia utalii nchini katika maeneo mbalimbali hususan wilaya ya Pangani.

Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah amesema, wilaya ya Pangani imejikita kwenye uwekezaji wa maeneo matatu ikihusisha utalii , kilimo mkakati na uchumi wa bluu na kuongeza kuwa wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya ya kimkakati yenye mazingira mazuri ya uwekezaji.

” Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji na tunawaomba wawekezaji kufika wilaya ya pangani kujionea fursa hizo muhimu “amesisitiza Zainabu

Uzinduzi wa mpango huo ulikwenda sambamba na Kongamano la uwekezaji chini ya maonyesho ya wadau wa Sekta ya Utalii kuunga mkono fursa za uwekezaji.

Wengine walioshiriki hafla hiyo ni Viongozi mbalimbali wa Serikali, watendaji wa taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo na wadau wa sekta ndani na nje ya nchi.

About Author

Bongo News

11 Comments

    Good day! Do you use Twitter? I’d like to follow you if that would be okay. I’m absolutely enjoying your blog and look forward to new updates.
    смотреть фильм

    Hi there! This is my 1st comment here so I just wanted to give a quick shout out and say I truly enjoy reading your articles. Can you suggest any other blogs/websites/forums that cover the same subjects? Thank you so much!

    https://ehl.org.ee/pag/codigo-promocional-de-1xbet.html

    Do you have a spam issue on this site; I also am a blogger, and I was wanting to know your situation; many of us have created some nice practices and we are looking to trade techniques with others, please shoot me an e-mail if interested.

    https://e-comex.com.ua/bi-led-linzy-dlya-avto-innovatsiynyy-pidkhid-do-osvitlennya

    Hey, I think your site might be having browser compatibility issues. When I look at your blog in Chrome, it looks fine but when opening in Internet Explorer, it has some overlapping. I just wanted to give you a quick heads up! Other then that, fantastic blog!

    https://ameli-studio.com.ua/perevahy-bi-led-linzy-dlya-avto-zbilshchyt-komfort-vodinnya

    For the reason that the admin of this website is working, no question very rapidly it will be well-known, due to its quality contents.
    https://xn--b1adgjdbhc1aebbqccldhhe2a7a.xn--p1ai/

    Its like you read my mind! You seem to know a lot about this, like you wrote the book in it or something. I think that you can do with a few pics to drive the message home a bit, but instead of that, this is fantastic blog. An excellent read. I will certainly be back.
    https://xn—–7kcgiiy1bf2ancu8h.xn--p1ai

    Hmm is anyone else encountering problems with the pictures on this blog loading? I’m trying to figure out if its a problem on my end or if it’s the blog. Any feedback would be greatly appreciated.
    ответ на игру words of wonders

    whoah this weblog is great i love reading your articles. Stay up the great work! You realize, lots of individuals are looking around for this info, you can help them greatly.

    Wyoming Valley Equipment LLC

    Kasyno Mostbet oferuje setki automatów i gier na żywo | Z Mostbet możesz zagrać na automatach, ruletce i w pokera | Dzięki Mostbet logowanie możesz grać w swoje ulubione gry w kilka sekund Mostbet logowanie kasyno

    Mostbet Polska to idealne miejsce na rozpoczęcie przygody z grami online | Sprawdź logowanie do kasyna Mostbet i graj bez ograniczeń | Mostbet kasyno oferuje darmowe spiny i turnieje z nagrodami Mostbet Polska – kasyno i zakłady

    Rejestracja szybka i intuicyjna – zyskałem bonus bez depozytu | Legalne kasyna i bukmacherzy z licencją, polecam sprawdzić | Szybki dostęp do logowania i promocji | Wszystko opisane prostym językiem, bez zbędnego żargonu | Bardzo dobre porównanie kodów promocyjnych | Funkcjonalna wyszukiwarka kodów promocyjnych | Bardzo przystępna nawigacja po serwisie | Możliwość rejestracji bez ryzyka – bonus bez depozytu | Kasyno online z najlepszym wyborem gier casino vulkan vegas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *