KITAIFA

RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI BARANI AFRIKA KUSHIRIKIANA KATIKA

RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI BARANI AFRIKA KUSHIRIKIANA KATIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni kuhusiana
na kazi mbalimbali ambazo Taasisi hiyo inafanya kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyasa uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 11 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema
moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo barani Afrika ni pamoja na janga la rushwa
ambalo linadhoofisha mifumo ya kitaasisi na kuathiri mipango na mikakati ya kujikomboa
kiuchumi.
Rais Samia amesema hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya
Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika na maadhimisho ya utekelezaji wa miaka 20
ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa yaliyofanyika
AICC.
Aidha, Rais Samia amesema viongozi wote barani Afrika hawana budi kuimarisha
ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa.
Vile vile, Rais Samia amewataka viongozi kutafakari na kuchambua kwa dhati masuala
ya rushwa ili kubainisha changamoto au vikwazo vya mapambano hayo na kuchukua
hatua muafaka.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kibajeti na kimfumo ikiwemo kuanzisha
taasisi zinazosimamia utawala bora na haki za binadamu nchini.
Rais Samia pia amesema Serikali imewekeza zaidi katika matumizi ya mifumo ya
TEHAMA inayosaidia kupunguza mawasiliano ya ana kwa ana katika kutoa huduma
kama michakato ya zabuni, usajili wa biashara na namba ya mlipa kodi ili kupunguza
mianya ya rushwa.
Kupitia Divisheni ya Mahakama Kuu inayosikiliza kesi za washtakiwa wa makosa ya
rushwa kubwa, Serikali imeokoa na kudhibiti matumizi ya fedha yasiyostahili ya zaidi ya
Shilingi bilioni 139 kuanzia mwaka wa fedha 2019/20 hadi 2021/22.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *