KIMATAIFA

WATALAAM WA SHERIA KUTOKA URUSI WATUA NCHINI KUELEZA UTAALAM NA UZOEFU WAO KATIKA KUPAMBANA NA UHALIFU WA KIMATAIFA

WATALAAM WA SHERIA KUTOKA URUSI WATUA NCHINI KUELEZA UTAALAM NA UZOEFU WAO KATIKA KUPAMBANA NA UHALIFU WA KIMATAIFA

Watalaam kutoka Ofisi kuu ya Waendesha Mashtaka Nchi Urusi wamewasili hapa Nchini kwa ajili ya kushiriki katika kongamano la kitaaluma litakaofanyika tarehe 30 Aprili 2024 katika shule ya uanasheria kwa vitendo Tanzania ( Law School) Jijini Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo Watalaam hao watatoa mada tatu ikiwa ni pamoja na kueleza namna ambavyo Wanasheria wa Shirikisho la Urusi wanavyofanya kazi, Utaalam na uzoefu wao katika kupambana na matukio ya uhalifu wa Kimataifa.

Hayo yameelezwa na Prof. Ambrose Kessy kutoka Shule ya Sheria Tanzania (Law School) alipowapokea watalaam hao jana usiku tarehe 27 Aprili 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema watalaam hao watashirikiana na Watalaam kutoka Shule ya Sheria Tanzania kuongelea mambo hayo; hivyo watu wote walio karibu ikiwemo Vyuo jirani na Taasisi ambazo zipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria wanaalikwa kushiriki.

Amesema Kongamano hilo litahudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pindi Chana, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Viongozi wengine mbalimbali.

“Itakuwa ni sehemu ambayo ni jumuishi kwa kweli kwa sababu litakuwa ni kongamano la kitaaluma kwa ajili ya kusogeza gurudumu la kuleta haki hapa Tanzania, kwa hiyo tunawaomba mshiriki nasi na pia kutoa fursa kwa Wananchi ambao wanaweza kututembelea kujua Law School inafanya nini” amesisitiza Prof.Ambrose Kessy.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *