Uncategorized KITAIFA

RC CHALAMILA ARIDHIA MAPENDEKEZO YA UGAWAJI WA BAADHI YA KATA NA MITAA KIGAMBONI

RC CHALAMILA ARIDHIA MAPENDEKEZO YA UGAWAJI WA BAADHI YA KATA NA MITAA KIGAMBONI

Asema mchakato wa Jambo hilo umefuata taratibu zote hitajika

  • Imedhihirika kuwa Kigamboni kwa sasa Kuna idadi kubwa ya watu
  • Asema hii itasaidia kupanua Maeneo ya Kiutawala
  • Wajumbe wote wa Kikao hicho wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni wafurahia kuungwa mkono kwa hoja hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila Novemba 29, 2023 ameridhia ombi la kugawa maeneo ya Kiutawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Kama yalivyowasilishwa

Chalamila amesema mchakato huo umefuata hatua zote stahiki ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo husika na kutembelea wananchi na viongozi Kisha kufanya mahojiano nao

Hata hivyo, RC Chalamila
Amepokea maoni mbalimbali ya Wajumbe hao ambapo kwa Umoja wao wamedhihirisha kuwa Kigamboni kwa sasa ina ongezeko kubwa la watu wanao hamia kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu

Vile vileMkuu wa Mkoa amesema utekelezaji wa Jambo hili utasaidia kupanua Maeneo ya kiutawala ya Kigamboni ambapo wananchi watapunguziwa umbali wa kwenda kupata huduma mbalimbali

Kwa upande wa Wajumbe wote wa kikao hicho wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Halima Bulembo wamefurahishwa na kupitishwa kwa mapendekezo ya kugawa baadhi ya kata na mitaa ya Kigamboni

Ikumbukwe kuwa Halmashauri hiyo kutokana na ukubwa wake na uhamiaji wa watu halmashauri hiyo imeona ni vema kuongeza idada ya kata kutoka 9 hadi kata 14 na Mitaa 67 hadi 77 ikiwa ni ongezeko la Kata 5 na Mitaa 10

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *