KITAIFA

WAPATA MAJI SAFI NA SALAMA BAADA YA MIAKA 50

WAPATA MAJI SAFI NA SALAMA BAADA YA MIAKA 50

Raisa Said,korogweWakazi 4,343 wa vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya Magila Gereza, wilayani Korogwe, kukamilika kwa mradi wa maji uliojengwa kwa  gharama ya Sh  775,743,809 million ni kukamlika kwa ndoto yao ya kuwa na maji safi na salama ya bomba ilidumu kwa zaiidi ya miaka 50.

Wakazi 4,343 wa vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya Magila Gereza, wilayani Korogwe, kukamilika kwa mradi wa maji uliojengwa kwa  gharama ya Sh  775,743,809 million ni kukamlika kwa ndoto yao ya kuwa na maji safi na salama ya bomba ilidumu kwa zaiidi ya miaka 50.

Kwa Mujibu wa Diwani wa Kata ya Magila Gereza Mwajuma Kitumpa amesema kuwa ndoto hiyo ilianza mnamo mwaka 1961 ambapo alisema walipata ‘kiashiria tu’ cha kupata maji. Ametanabahisha, kwa mujibu wa wazazi wao, kuwa walikuja wataalamu mwaka huo kupima maji katika eneo hilo.

“Baada ya hapo hawakuonekana tena na imekuwa hadithi hadi mwaka jana 2023 ambapo walipata tena viashiria vya ndoto hiyo kuwa ya kweli,” alisema Diwani Kitumpa

Diwani huyo amesema kuwa mradi huo ni ukombozi kwa wanawake ambao alisema walikuwa wanalazimika kwenda mbali kuchota maji mahali ambapo walikutana na changamoto kadhaa wa kadha ikiwa ni pamoja na vitisho kutoka kwa vijana wakorofi ambao walikuwa wanawanyanyasa.

Pia alizungumzia migogoro na waume zao ambao ambao walikuwa hawapendezwi kuachwa kitandani saa kumi usiku na wake zao licha ya kwamba walikuwa wanatafuta maji kwa ajili ya familia.

“Kuna madimbwi huko katikati ya misufi ambako watu walikuwa wanachota maji na kuweka waterguard ili yabadilike. Sasa hivi wanafurahia kwa sababu hata foleni hakuna kutokana na kuwa vilula vingi huko vijijni,” alisema Diwani.

Mradi umwjwnga tenki la maji lenye uwezo khhifadhi lita 300,000 na kujenga virula 28 na l kulaza mabomba yenye urefu wa kilometa 16,000.

Alimpongeza Rais Samia kwa kuwakomboa  wanawake na kuwatua ndoo kichwani na kufanya tatizo la maji kuwa historia katia kata ya Gereza. “Sasa hivi mpango wetu ni  kuanza mpango wa kupeleka maji nyumbani baad ya mradi kukabishiwa chombo cya watumiaji Maji.,” alisema Diwani.

Naye Monica Julius, mkazi wa Kijiji cha Kalekwa alisema kuwa wamekuwa wakipata taabu kutoka usiku kwenda kuchota maji msituni mbali. “Tumevumulia kufukuzwa na majambazi na mpaka hivi sasa tuna maji. Hata waume zetu sasa wanafurahi wanasema kuwa ndoa zetu sasa zitadumu. Tunashukuru viongozi, hasa mama yetu Samia ametutua ndoo kichwani,”alisema Bi Julius.

Naye George Cyprian Singano, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kalekwa ambaye alisema kuwa wananchi wanachota maji hawaendi mbali.

“Maji tuliyokuwa tunatumia yalikuwa yanatoka Mlima Sindei ambako watu kule wanalima tangawizi na wanatia madawa hivyo tulikuwa tuna pata magonjwa mengi kama vile ugonjwa wa kuhara,’ alisema.

Hata hivyo alisema kuwa serikali inapaswa kufuata ratiba na alipendekeza wasiweke lengo la karibu ili waweze kuondoa matumaini makbwa ya wananchi na kuepuka maswali wakati lengo linaposhindwa kutimizwa.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *