BURUDANI

WAZIRI DKT. CHANA AFUNGUA TAMASHA LA PILI LA UTAMADUNI, NJOMBE YANEEMEKA

WAZIRI DKT. CHANA AFUNGUA TAMASHA LA PILI LA UTAMADUNI, NJOMBE YANEEMEKA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amefungua
Tamasha la pili la kitaifa la Utamaduni Agosti 25, 2023 katika viwanja vya Stendi ya
zamani mkoani Njombe.

Katika Tamasha hilo wananchi wa Mkoa wa Njombe wameendelea kupata burudani na
fursa ya kuuza na kuonesha bidhaa zao, huku mikoa mbalimbali iliyohudhuria tamasha
hilo kupitia vikundi na Sanaa na ngoma vikionesha Utamaduni na kuuza kazi zao za
ubunifu.

Akifungua Tamasha hilo Waziri Mhe. Pindi Chana amesema tamasha hilo ni utekekezaji
wa Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ambayo inatoa fursa kwa jamii kuenzi na
kulinda mila na desturi pamoja na kuzirithisha kwa vizazi cha sasa na vijavyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa
amesema Tamasha hilo limetoa fursa kwa wananchi wa Njombe hatua inayowaongezea kipato katika biashara zao, kuona utamaduni wa mikoa mingine pamoja na kuonesha kuonesha utamaduni wao.

Awali akitoa maelezo juu ya tamasha hilo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Saidi
Yakubu amesema tamasha hilo ni utekekezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa Septemba mwaka
2021 mkoani Mwanza, lengo likiwa ni kurithisha Utamaduni, mila na desturi za makabila yote Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kutangaza Utamaduni wa Mtanzania.

Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema Tamasha hilo linajumuisha mashindano ya ngoma
za asili, vyakula, maonesho ya flamu ikiwemo za Harakati za Ukombozi wa Bara la
Afrika, kuitangaza Royal Tour, Mada mbalimbali kuhusu maadili na utamaduni pamoja
na huduma ya upimaji wa afya na elimu ya lishe, uchangiaji wa damu pamoja na
kuwepo kwa mechi za kirafiki na matembezi mafupi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *