KITAIFA

WAZIRI KAIRUKI APOKEA MATOKEO YA SENSA YA WANYAMAPORI ARUSHA

WAZIRI KAIRUKI APOKEA MATOKEO YA SENSA YA WANYAMAPORI ARUSHA

Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Angellah Kairuki anaongoza hafla maalum ya kutangaza matokeo ya Sensa ya wanyamapori na kuzindua ripoti na taarifa ya watalii waliotembelea nchini Tanzania mwaka 2023.

Wizara ya Maliasili na Utalii inasema lengo la kufanya Sensa hiyo ya wanyamapori ni kuhakikisha uhifadhi endelevu na kutoa takwimu sahihi juu ya uwepo, idadi na mtawanyiko wa wanyamapori.

Lengo lingine kulingana na Wizara ya Maliasili na Utalii ni pamoja na kuendeleza na kukuza utalii pamoja na kupunguza migogoro baina ya binadamu na wanyamapori.

Mheshimiwa Felician Mtahengerwa, Mkuu wa wilaya ya Arusha anamuwakilisha Mheshimiwa Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Arusha kwenye hafla hiyo inayofanyika kwenye Ukumbi wa Gran Melia leo Aprili 22, 2024.

Hafla hii inafanyika mkoani Arusha wakati huu ambapo Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda anatekeleza mikakati mbalimbali katika utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kukuza utalii mkoani hapa pamoja na kuboresha na kujenga malazi ya kutosha ili kuhudumia wageni na watalii wanaofika mkoani Arusha.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *