KITAIFA

BAKWATA IMEWAUNGANISHA WAISLAMU WOTE

BAKWATA IMEWAUNGANISHA WAISLAMU WOTE

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaj Nuhu Jabir Mruma amesema, kwa takribani miaka nane ya uongozi wa Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally, BAKWATA imewaunganisha Waislamu wote nchini na kuwa kitu kimoja.

Alhaj Mruma ameyasema hayo wakati akihutubia Baraza la Eid Al Adha lililofanyika kitaifa katika Msikiti wa Mohammed VI Kinondoni, Dar es Salaam na kuwataka Waumini wa dini ya Kiislamu nchini kuendelea kuwa kitu kimoja.

“Sio jambo zuri mbele ya Allah (S.W), Waislamu kufarakana. Kama sisi wenyewe Waislamu tunanyoosheana vidole kwa misingi ya madhehebu, au kwa hila tu za kilimwengu, basi tuelewe kuwa tutakuwa masuhuli mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiama kwa kuudhoofisha Uislamu”. Amesema Alhaj Mruma

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *