KITAIFA

BANDARI MWANZA KUSINI KUFANYIWA MABORESHO YA NGUVU

BANDARI MWANZA KUSINI KUFANYIWA MABORESHO YA NGUVU

Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Ferdinand Nyathi akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)

Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Ferdinand Nyathi amesema kuwa, baada ya maboresho ya baadhi ya bandari za ukanda huo, kinachofuata sasa ni maboresho ya Bandari ya Mwanza Kusini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika bandari hiyo Mei 31, 2023, Meneja huyo amesema kuwa kuna stadi inafanyika kwa ajili ya maboresho hayo, itakapokamilika kazi itaanza, kwani bandari hiyo inategemewa zaidi katika kusafirisha shehena mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Bandari ya Mwanza Kusini ipo eneo la Igogo, Wilaya ya Nyamagana, eneo lake lina ukubwa wa hekta 12, huku eneo la kuhudumia meli likiwa na takribani mita 210. Ina miundombinu mbalimbali pamoja na eneo la kuhifadhia mizigo, kuna reli ya kati inangia bandarini kwa ajili ya kuhudumia mizigo.
“Bandari yetu hii inahudumia mizigo inayotoka na kwenda nje ya mipaka ya Tanzani, tunapata meli kutoka Uganda, Kenya na kwingineko. Ndio bandari kubwa kwa maana ya kuhudumia shehena kubwa,” alisema.
Kipekee tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassan kwa jitihada ambazo inafanya kuhakikisha kwamba nchi yetu inatengeneza uwezo mkubwa sana kwa maana ya miundombinu rafiki kwa ajili ya kuchachusha hii biashara kati ya taifa letu pamoja na nchi Jirani, tunaona mazingira yanayotengenezwa kwa sasa ni rafiki, mataifa yanatembelea na yanajadiliana jinsi ya kuboresha maeneo mbalimbali. Kwa hiyo hiki ni kitu ambacho kwakweli kinasaidia sana,” alisema

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *