MICHEZO

TANZANIA NA JAPAN KUSHIRIKIANA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

TANZANIA NA JAPAN KUSHIRIKIANA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kulia)
akisalimiana na Mtaalamu wa michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA)
Dkt. Shiraishi Tomoya (kushoto) Juni 01, 2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema
Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) katika
sekta ya michezo nchini ili kuendelea kutoa ajira kwa watu wengi zaidi hatua
inayosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Bw. Yakubu amesema katika kikao chake na Mtaalamu wa michezo kutoka Shirika la
Maendeleo ya Japan (JICA) Dkt. Shiraishi Tomoya Juni 01, 2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (wa tatu
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka utoka Shirika la Maendeleo ya
Japan (JICA) wakiongozwa na Mtaalamu wa michezo Dkt. Shiraishi Tomoya (wa pili
kushoto) Juni 01, 2023 jijini Dodoma.

“Uwepo wako hapa nchini utasaidia wananchi kuwaokoa na watu wengi na magonjwa
yasiyoambukiza, Rais yupo mstari wa mbele katika michezo, naamini uwepo wako hapa
nchini butasaidia kukuza michezo na kuifanya kuwa maarufu na watu wengi kushiriki”
amesema Bw. Yakubu.

Kwa upande wake Dkt. Shiraishi Tomoya amesema anauzoefu wan chi za Afrika
Mashariki na anaiona michezo katika miaka 10 ijayo michezo inakuwa sehemu ya jamii
ambapo watu wote watashiriki na kuimarisha afya zao.

Dkt. Shiraishi Tomoya ni mtaalamu na mshauri wa michezo na maendeleo atakuwepo
nchini na kufanya kazi katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na atakuwa nchini kwa
muda wa miaka mitatu kutoka 2023 hadi 2027.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *