KITAIFA

KINAMAMA EPUKENI KAUSHA DAMU- MHE. UMMY

KINAMAMA EPUKENI KAUSHA DAMU- MHE. UMMY

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akikabidhi mitungi ya gesi kwa vikundi vya  wanawake Wilaya ya Moshi Mjini wakati wa ziara yake katika Mkoa huo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro ambaye  pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga  amewatahadhalisha wanawake kutochukua mikopo itakayowarudisha nyuma kimaendeleo maarufu Kausha damu.

Mhe. Ummy ameyasema hayo alipotembelea Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro zikiwemo Wilaya za Moshi Mjini na Siha na kuzungumza na Baraza la Wanawake la Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na vikundi vya wanawake ambapo amewasihi wanawake kuwa makini pindi wanapoamua kuchukua mikopo hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (aliyesimama) akizungumza na Baraza la Wanawake la Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Mjini wakati wa ziara yake katika Mkoa huo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ina nia njema ya kuhakikisha kina mama wanajikwamua kiuchumi kupitia asilimia 10% ya mikopo inayotolewa na kila Halmashauri.

“Utaratibu wa mikopo  hiyo  utakaporejeshwa kina mama wapewe kipaumbele na mfanye shughuli za maendeleo halafu  kina mama wa mjini tuache kukopa mikopo ya kausha damu  kwasababu ni mibaya wakati mwingine inavunja ndoa kwahiyo kabla ya kukopa omba ushauri usiingie kwenye madeni na kupata fedheha,”Amesema Mhe. Ummy.

Kuhusu Ilani ya Chama Cha Mapinduzi amebainisha kuwa imeendelea kutekelezwa katika sekta mbalimbali kuhakikisha wananchi  wanapata  maendeleo  huku akitoa onyo kwa baadhi ya watu wasiyo na nia njema na Serikali kuacha kubeza juhudi za  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akikabidhi mitungi ya gesi kwa vikundi vya  wanawake Wilaya ya  Siha  wakati wa ziara yake katika Mkoa huo.

“Tuendelee kuungana mkono, tuendelee kukisemea Chama kwasababu ilani ya Chama inatekelezwa vizuri na kazi inaendelea kina mama tutembee kifua  mbele  kina mama  tunaye Mhe. Rais Dkt. Samia jasiri na jemedari anafanya kazi kubwa na nzuri,” Amebainisha Mhe. Ummy.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Mkoa wa Kilimanjaro Ndug. Elizabeth Minde amewahimiza watanzania kuendelea kuheshimu na kulinda Amani ya Nchi iliyopo kwa kuepuka kutumiwa na  baadhi ya watu wasiyo na nia njema na Taifa la Tanzania.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amegawa mitungi ya gesi kwa vikundi vya wanawake Wilaya ya Moshi Mjini na Wilaya ya Siha kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya safi ya kupikia na kuepuka matumizi ya kuni na mkaa ili kuhifadhi mazingira.

“Hatuhitaji Nchi yetu kuingia katika migogoro mikubwa itakayofanya watu wasitulie kutekeleza shughuli za kimaendeleo tunahitaji maendeleo  kwa sababu inapotokea migogoro kina mama, watoto, wazee na watu wenye ulemavu ndiyo wanaoathirika zaidi, “ Ameeleza Mwenyekiti huyo.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro Dkt. Christopher Timbuka amewataka kina mama kupaza sauti zao kupinga vitendo vya ukatili katika jamii na uvunjifu wa maadili badala ya kuwa sehemu ya kuwaficha wanaofanya vitendo hivyo hatua inasababisha kuongeza kwa matukio ya kikatili.

“Wilaya ya Siha inaongoza kwa vitendo vya ukatili  na shida kubwa ya Siha ni kufichiana siri wakati tunaamini kina mama ni jeshi kubwa naomba tutoe ushirikiano kuzuia vitendo vya kikatili na mmomonyoko wa maadili  kwa kutoa taarifa za wanaofanya vitendo hivyo,”Amehimiza Dkt. Timbuka.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *