KITAIFA

MAKAMBA AGAWA MAJIKO 123 YA GESI KWA SHULE ZA BUMBULI

MAKAMBA AGAWA MAJIKO 123 YA GESI KWA SHULE ZA BUMBULI

Raisa Said,bumbuli
Mbunge wa Jimbo la bumbuli January Makamba ametoa msaada Wa majiko ya gesi 123  katika shule za Sekondari 24 na Msingi 99 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mkoani Tanga.

Msaada huo umetolewa wakati Wa kikao Cha tathimi ya elimu  na wakati wakupongeza shule zilizofanya  vizuri Mwaka 2023  nazilizotoa wanafunzi  waliofanya vizuri katika mitihani ya darasa la Saba mwaka Jana.

Makamba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje ametoa mitungi hiyo ya gesi  kuunga mkono juhudi za Rais Samia ambaye ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia gesi safi ya kupikia.

Wakipokea majiko hayo ya gesi walimu hao yaliyokabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Amir Shehiza na Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Baraka Zikatimu walisema wanashukuru kwa kupata msaada huo ambao umekuja wakati muafaka kwao.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *