KITAIFA

KIKWETE AFURAHISHWA NA UBUNIFU WA WALENGWA WA TASAF NA VIONGOZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA KWA KILIMO CHA KISASA

KIKWETE AFURAHISHWA NA UBUNIFU WA WALENGWA WA TASAF NA VIONGOZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBAHA KWA KILIMO CHA KISASA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama miti ya mbogamboga katika shamba darasa la kilimo cha kisasa kinachotekelezwa na kikundi cha walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema moja kati ya mbinu ambazo Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
amekuwa akisisitiza kwa wananchi wote ni kushiriki katika kubuni mbinu
mbalimbali zitakazowawezesha wananchi kujimudu na kuendesha maisha
yao pasipokuwa na changamoto yoyote.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Mhe. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na
walengwa wa TASAF wa Kata ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Mhe. Kikwete amesema kuwa, Rais Dkt. Samia amekuwa akitoa fedha
nyingi ili ziweze kutumika kupitia mbinu na ubunifu mkubwa wenye ubora ili
kuweza kuwainua wananchi kiuchumi.

Sehemu ya wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza nao alipokuwa kwenye ziara ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.


Mhe. Kikwete ametoa pongezi kwa wananchi na watendaji wakiwemo
viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kuhakikisha
utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya miradi ya TASAF inatekelezeka
kupitia kilimo cha kisasa.
Mhe. Kikwete amesema tangu aanze ziara za kikazi katika baadhi ya
mikoa amekuwa akikutana na shuhuda na bunifu wa vitu mbalimbali hivyo
ni dhahiri kuwa wananchi na walengwa wa TASAF wamekuwa wakifaidika
kupitia bunifu za vitu mbalimbali.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon
amesema wananchi wa taifa la Tanzania ni watu wenye ukarimu hivyo ni
vizuri wakaendelea kushirikiana kwa kuwainua walio chini na kupitia mradi
wa TASAF jambo ambalo linatekelezeka kwa asilimia kubwa.

Mwonekano wa kilimo cha kisasa cha nyanya kinachotekelezwa na kikundi cha walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.

Naye, Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Sijaona
Muhunzi amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wanatekeleza
miradi mbalimbali ikiwemo ajira za muda, mradi wa kuweka akiba na
kukuza.
Katika hatua nyingine, Mhe. Naibu waziri Kikwete amefanya kikao kazi na
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Kibaha ambapo amewataka
watumishi wa halmashauri hiyo kujiwekea malengo ya utendaji kazi ili
kuboresha kazi zao kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete anaendelea na ziara ya kikazi ya wiki moja
katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa
umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao pamoja na
kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *