KITAIFA

NDEJEMBI ATAKA MAENEO YA KUJENGA SHULE YATENGWE KUKIDHI MAHITAJI

NDEJEMBI ATAKA MAENEO YA KUJENGA SHULE YATENGWE KUKIDHI MAHITAJI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mara baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Liwiti inayojengwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mradi wa SEQUIP.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Deogratius Ndejembi amesema kuna ulazima wa kutenga maeneo kwa ajili
ya ujenzi wa shule ili kukidhi mahitaji yanayotokana na ongezeko la
wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto wa wanafunzi kutembea
umbali mrefu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akipanda mti katika shule ya Msingi Kunduchi, mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa kupitia mradi wa BOOST katika shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.


Mhe. Ndejembi ametoa wito huo akiwa mkoani Dar es Salaam, wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu
inayojengwa kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP katika Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Mhe. Ndejembi amesema maeneo hayo yakitengwa, kuna ulazima wa
kujenga shule za ghorofa badala ya majengo ya chini ili kutatua
changamoto ya kukosa viwanja vya michezo vya watoto ambavyo ni
muhimu kwa ajili ya kujenga afya ya akili.
“Michezo ni muhimu kwa ajili ya afya ya akili na makuzi ya watoto hivyo ni
lazima kuwepo na ushirikiano wa viongozi kuanzia ngazi ya mtaa, kata,
halmashauri, wilaya na mkoa katika kuhakikisha shule zinajengwa kwenda
juu ili kupata maeneo ya viwanja vya michezo,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya
kuboresha elimu ya msingi na sekondari, hivyo ni lazima kuendelea
kutenga maeneo ya ujenzi na kuyatumia vizuri ili yawe na tija.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na walimu, wananchi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Boma yanayojengwa kupitia mradi wa BOOST kwenye halmashauri hiyo.


Aidha, Mhe. Ndejembi ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kukamilisha ujenzi wa
shule mpya na ukarabati wa miundombinu ya elimu, kupitia fedha za mradi
wa BOOST na SEQUIP zilizopatikana kutokana na jitihada za Rais Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kuendelea kuboresha
miundombimu ya elimu nchini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule
amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za

ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia mradi ya BOOST na SEQUIP na
kuahidi kuendelea kusimamia vizuri matumizi ya fedha hizo ili ziwe
manufaa kwa taifa.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *