KITAIFA

MKUU WA MKOA DODOMA: KAMILISHENI MICHORO YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI MPWAYUNGU KWA WAKATI

MKUU WA MKOA DODOMA: KAMILISHENI MICHORO YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI MPWAYUNGU KWA WAKATI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Msuya wakikagua eneo la Ujenzi wa Shule mpya ya
Sekondari Mpwayungu katika ziara iliyofanyika tarehe mwishoni mwa wiki, Wilayani
Chamwino.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameagiza wakandarasi
wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Mpwayungu iliyopo
Wilayani Chamwino kukamilisha michoro ya ujenzi huo ili kuwezesha kazi
nyingine kuendelea.
Mhe. Senyamule ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara yake ya
kikazi katika Wilaya hiyo katika Kata ya Mpwayungu ambapo ametembelea
miradi kadhaa ikiwemo Ujenzi wa Shule hiyo, Mradi wa kupambana na Ujangili
na biashara haramu ya Wanyamapori katika mfumo wa ikolojia wa hifadhi za
Ruaha [WMA] katika kijiji cha Ndogowe na Mradi wa Kilimo cha Pamoja (BBT)
Amesema kuwa iwapo michoro hiyo itakamilika kwa wakati itatoa fursa kwa
wananchi kuendelea na zoezi la kuchimba msingi ndani ya wiki moja.

Kwenye Picha ni baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mlazo na Ndogowe wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa mkutano wa
hadhara na wakazi wa eneo hilo. Senyamule alitumia hadhara hiyo kusikiliza kero za
wananchi na kuwaeleza vipaumbele vya Serikali.


Mhe. Senyamule ameelekeza Watendaji kuhakikisha wanasimamia kazi zinazo
wahusu ikiwemo Uchimbaji wa msingi, kusogeza kokote ,vifusi vya mchanga ili
mradi huo uweze kwenda kasi na kukamilika kwa wakati.
” Natarajia kuona uchimbaji wa msingi umekamilika ndani ya siku saba na
kufanya hivyo ni ishara ya kwamba mnauhitaji wa uharaka wa maendeleo kwani
serikali inahitaji kasi na ufanisi” ameeleza Senyamule
Aidha amesema kuwa kiasi cha Fedha zaidi ya Shilingi milioni 544
zimeshatolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo japo kasi ya utekelezaji ni
ndogo, hivyo ametoa rai kuongeza kasi ili ifikapo tarehe10/10/2023 mradi uwe
umekamilika.
Mradi huo unahusisha Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 8, Jengo la Utawala ,
Maktab, Chumba cha Tehama ,Matundu ya vyoo vya wanafunzi 8, Maabara ya
Sayansi 3, Tanki la Kuhifadhia maji moja la Lita 32000 , Kichomea taka na
jenereta vinavyotekelezwa chini ya ufadhili wa Fedha za SEQUIP.
Katika hatua nyingine Mhe. Senyamule akiwa kwenye Mkutano wa hadhara na
wananchi wa kijiji cha Mlazo na Ndogowe amesisitiza wananchi kujitokeza
kushiriki kwa kutoa nguvu kazi kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari
Mpwayungu
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan
ameelekeza kila Kata kuwa na Shule ya Sekondari amefanya jitihada na
anaendelea kutupatia fedha kwa ajili ya kutengeneza Miundombinu wezeshi kwa

watoto ili maendeleo ya mguse kila mmoja hivyo tushirikiane kuunga mkono
jitihada hizo.” Ametoa wito Mhe. Senyamule
Hata hivyo, Mhe.Senyamule amekemea vikali suala la Utoro wa watoto Shuleni
na hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa wazazi wazembe kufutilia mienendo
ya watoto wao na wengine wanaobaki nyumbani kwa ajili ya shughuli za
nyumbani na hivyo kupelekea watoto hao kuto maliza masomo.
“Tutafutilia lazima tutahakikisha mtoto mmoja mmoja anapata haki yake ya
msingi ya kupata Elimu na kuwachukulia hatua kali kwa wazazi watakao bainika
wanachangia watoto wao kuwa watoro Shuleni “amesisitiza Senyamule
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Gift Msuya amesema kuwa ujenzi wa
Shule hiyo umezingatia vigezo vyote ikiwemo umbali kwa wanafunzi na
kuwataka wakazi wa kata hiyo kubadilika kwani maendeleo hayajaribiwi
washirikiane ili kusogea mbali kuitekeleza kesho .
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma Mwl. Gift Kyando
amewataka
wakandarasi wanaohusika na Ujenzi wa Shule hio kutoharibu mazingira kwa
kukata miti ovyo .
Mwalimu Kyando ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kutoa ushirikiano pindi
ujenzi unavyoanza sambamba na kutumia fursa zilipo kwa muda wa utekelezaji
wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika Kata hiyo.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *