KITAIFA

SIMANZI, VILIO VYATAWALA MWILI WA MTANZANIA ALIYEUAWA NCHINI ISRAEL UKIWASILI NYUMBANI KWAO ROMBO

SIMANZI, VILIO VYATAWALA MWILI WA MTANZANIA ALIYEUAWA NCHINI ISRAEL UKIWASILI NYUMBANI KWAO  ROMBO

Simanzi vilio na huzuni imetawala Katika kijiji cha Kirwa Wilaya ya Rombo,mkoani Kilimanjaro baada ya mwili wa marehemu Clemence Mtenga (22) Mtanzania aliyeuawa nchini Israel ukiwa umewasili nyumbani kwao

Bongonews imeshuhudia msafara wa kuutoa mwili katika hospitali ya huruma ulikokuwa umehifadhiwa, ukiongozwa na mkuu wa kituo cha polisi (OCD) Rombo hadi nyumbani na ulibebwa na askari wa jeshi la akiba (Mgambo)

Imefahamika kuwa Mwili wa Mtengwa hautaonyeshwa kutokana na mazingira ya mwili na kwamba waombolezaji wataaga kwa kuangalia picha juu ya jeneza.

Mwili uliwasili nchini jana Novemba 27, 2023, saa 2:51 usiku, kwa ndege ya shirika la KLM kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu aliyekuwa ameongozana na kamati ya usalama.

Novemba 17, Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilithibitisha kupokea taarifa za kifo cha Clemence Mtenga, miongoni mwa watanzania wawili ambao pamoja na raia wa mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo baada ya kuanza kwa vita kati ya Hamasi na Israel.

Taarifa hiyo iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano ya serikali cha Wizara hiyo, ilieleza Clemence alikuwa miongoni mwa vijana wa kitanzania 260, waliokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo, chini ya mpango wa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Israel.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *