Uncategorized

UJENZI BARABARA YA LUPETA-WIMBA-IZUMBWE KUINUA UCHUMI WA MBEYA

UJENZI BARABARA YA LUPETA-WIMBA-IZUMBWE KUINUA UCHUMI WA MBEYA

Mbeya

Ujenzi wa barabara ya Lupeta-Wimba -Izumbwe yenye urefu wa Km.9.5 na ile ya Inyala-Simambwe Km. 16.7 kwa kiwango cha lami imelenga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi mkoani Mbeya kwa kurahisisha usafirishaji wa mazao kwa urahisi.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dennis Londo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya elimu na miundombinu ya Barbara mkoani Mbeya.

Mhe. Lundo alisema kuwa kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja chini ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

“Kazi kubwa na yenye viwango imefanyika katika elimu na miundombinu katika Halmashauri hii, Miradi hii miwili ya barabara tuliyotembelea ni muhimu kwa uchumi wa Mbeya lakini na Taifa kwa ujumla”Alisema Mhe. Londo

Kwa upande wa uchumi Mhe. Londo alisema barabara hizo zitaeda kurahisisha shughuli za kilimo na kupunguza gharama za pembejeo na uzalishaji kwani gharama za usafirishaji zitapungua, hivyo kumuongezea kipato mkulima mmoja mmoja na kumuondolea umaskini mwananchi.

Naye, Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila alisema wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yote.

Wakati huo huo Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TARURA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Barabara Mhandisi Venant Komba alisema kuwa katika Mkoa wa Mbeya TARURA inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya barabara zinazofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya chini ya mradi wa Agri Conect.

Mhandisi Komba alisema kuwa kwa barabara ya Lupeta-Wimba ipo katika hatua za mwisho na itakamilika katikati ya mwezi Februari, mwaka huu.

Agri Connect ni mpango unaotekelezwa na TARURA kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na madhumuni ya ujenzi ni kukuza uchumi wa Mkoa pamoja na nchi kwa ujumla, kuchochea maendeleo ya sekta binafsi, kutengeneza ajira kwenye sekta ya kilimo na kuongeza thamani ya mazao ya biashara yaliyopo ndani ya Mkoa.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *