KITAIFA

HABARI PICHA; RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MINARA YA KURUSHIA MATANGAZO YA TELEVISHENI ARDHINI

HABARI PICHA; RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MINARA YA KURUSHIA MATANGAZO YA TELEVISHENI ARDHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media kwenye hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi hizo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi wa Azam Media mara baada ya kufungua Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.

Wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Minara ya kurushia matangazo ya Televisheni
Ardhini (DTT) iliyofanyika katika Ofisi za Azam Media, Tabata Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited Ndugu Tido Mhando wakati alipotembelea Studio za matangazo za Azam TV zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Mama Eda William Sanga, Mtangazaji wa kwanza Mwanamke kutangaza Taarifa ya habari ya Tanzania kupitia Redio Tanzania (RTD) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) Tabata Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mtoto Georgina Magesa (8) mara baada ya kuonana na Mhe. Rais katika Ofisi za Azam Media zilizopo katika Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2023.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *