KITAIFA

RAIS SAMIA ASHIRIKI KILELE CHA SHEREHE ZA NANENANE

RAIS SAMIA ASHIRIKI KILELE CHA SHEREHE ZA NANENANE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa
na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa
Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Mweli pamoja na Dkt. Hussein Mohammed Omar Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya maafisa ugani, trekta kwa wakulima, vifaa vya kutengeneza Vihenge vya chuma kwa Vijana, beielekezi za mbolea ya ruzuku, mradi wa uchimbaji wa visima pamoja na ugawaji wa vifaa vya mfumo wa umwagiliaji kwa matone katika Maonesho ya
Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya tarehe 8 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa
wito kwa wakulima kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha na kuuza ziada kupitia
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili wapate faida.
Rais Samia ametoa wito huo leo kwenye kilele cha maonesho ya kilimo na
maadhimisho ya sherehe za Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John
Mwakangale.
Aidha, Rais Samia amesema Serikali imedhamiria kuwa na uwezo wa kuhifadhi
chakula tani 3,000,000 ifikapo mwaka 2030 ili ziweze kusaidia nyakati za dharura.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amesema serikali inaendelea kufanya jitihada
za makusudi za kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika kilimo kwa kuwa
kundi hilo ndilo nguzo muhimu kwa uchumi wa taifa.
Rais Samia pia amesema jitihada hizo ni pamoja na kuanzishwa kwa Programu ya
miaka 8 inayoitwa Building a Better Tomorrow ( BBT) ambapo vijana 812 (wanawake
282 na wanaume 530) wanaendela na awamu ya kwanza ya mafunzo ya kilimo
biashara katika vituo atamizi 13.
Vile vile, Rais Samia amesema juhudi hizi zimeifanya Tanzania kutambulika
kimataifa na kuchaguliwa kuwa Mwenyeji wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani
Afrika (African Food Systems Forum) litakalofanyika tarehe 5 -8 Septemba mwaka
huu jijini Dar es Salaam.
Halikadhalika, Rais Samia amesema Jukwaa hilo litaipatia Tanzania fursa za
kibiashara na kuongeza ushirikiano na nchi za Afrika, kwa kuwa na mifumo jumuishi
ya kuimarisha kilimo, mifugo na uvuvi itakayochochea zaidi ajira, uwekezaji na
ukuaji wa uchumi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *