MICHEZO

UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR WAKAGULIWA MAANDALIZI YA AFCON 2027

UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR WAKAGULIWA MAANDALIZI YA AFCON 2027

Timu ya Wakaguzi ya utayari wa nchi za Kenya Uganda na Tanzania kuhusu utayari
wao wa kuwa wenyeji AFCON 2027, leo hii Julai 31, 2023 wapo Zanzibar ambapo
wamekagua Uwanja wa Amaan, hospitali ya Mnazi Moja, Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Aman Karume pamoja na viwanja vingine vya mazoezi.

Timu hiyo kutoka Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) imezungukia maeneo hayo
ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi
Yakubu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Wallace Karia na Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar Bw Suleiman Mahamud Jabir.

Maafisa wengine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo
Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Bw. Ally Mayayi na Katibu Mtendaji Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha na kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni Kamishna
Idara ya Michezo Bw, Ameir Mohammed, Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar
Saidi Marine pamoja na maafisa wengine kutoka TFF na ZFF.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *