KITAIFA

RC CHALAMILA AKUTANA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA DAWASA NA TANESCO

RC CHALAMILA AKUTANA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA DAWASA NA TANESCO

Akiongea wakati wa kikao hicho RC Chalamila amezitaka Taasisi hizo mbili kufanya kazi kwa kushirikiana, pamoja na kuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi ili kuwa na uzalishaji wenye tija utakaopelekea kutoa huduma bora kwa Jamii wakati wote

Aidha RC Chalamila amesema Dar es Salaam ni hub ya kibiashara, hub ya kidiplomasia, hub ya kiuchumi na vingine vingi,vinavyofanana na hivyo, umeme au maji vikikosekana kuna hatarii kubwa ya kudhorota kwa mnyororo mzima wa uchumi wa nchi.

” Natamani kuona Mkoa wa Dar es Salaam hauna changamoto au migao ya aina yoyote ya umeme wala maji kutokana na umuhimu wa Mkoa huu katika makuzi ya uchumi wa nchi” Alisema RC Chalamila

Sambamba na hilo RC Chalamila amesema umeme ukiwepo maji huzalishwa kwa wingi na maji yakizalishwa kwa wingi husaidia kwa sehemu kubwa kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *