MICHEZO

RC CHALAMILA “SIJARIDHISHWA NA KASI YA MKANDARASI UWANJA WA MPIRA MWENGE”

RC CHALAMILA “SIJARIDHISHWA NA KASI YA MKANDARASI UWANJA WA MPIRA MWENGE”

Mhe Albert Chalamila amesema hayo leo Februari 17,2024 wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo ambapo amemtaka Mkandarasi Group six International kabla ya machi 30, 2024 awe amekamilisha ujenzi huo na uwanja uanze kufanya kazi mara moja.

Aidha RC Chalamila amekemea vikali wakandarasi wasio na uwezo na wanachelewesha kazi kuanzia sasa hawatapatiwa kazi zingine katika Mkoa huo

Vilevile RC Chalamila ameelekeza uwanja huo ufanyiwe maboresho ikiwemo sehemu za VIP lakini pia sehemu za kukaa watanzamaji zitengenezwe vizuri zivutue na sio kuweka mbao vilevile uwanja ukikamilika uwe na huduma za mtandao kwa kuweka Free Wifi

Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo pamoja na Mstahiki Meya kwa niaba ya madiwani wamesema Manispaa hiyo haina mkwamo wowote wa kifedha, fedha zipo Changamoto kubwa ni mkandarasi na wao matarajio yao ni kuona awamu ya pili KMC FC wangeanza kutumia uwanja huo

Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amesema uwekezaji unaofanywa na Wilaya hiyo umelenga kupanua fursa za ajira pamoja na mapato kwa masilahi mapana ya Wananchi.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *